Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Hasan Jafari, Katibu Mkuu wa Chama cha Ustawi wa Kitaifa cha Afghanistan, katika kuelezea mauaji ya kigaidi dhidi ya viongozi wakuu wa serikali ya Yemen, alitoa tamko rasmi, katika tamko hilo, huku akiipa pole Harakati ya Ansarullah na watu wa Yemen, aliliita tendo hili “alama ya kudhalilika na kukata tamaa” kwa utawala wa Kizayuni mbele ya mapambano ya Wayemen, J'afari, akilaani kwa ukali jinai hiyo, alisisitiza haja ya ulimwengu wa Kiislamu kufanya maamuzi makubwa na kuchukua hatua za haraka za Umoja wa Mataifa kusitisha “mauaji ya halaiki,” na akaonya kwamba endapo hakutakuwa na mwitikio, tutaona uvamizi wa Israeli dhidi ya nchi nyingine za Kiislamu.
Matini kamili ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mola wa mashahidi na wasadiki
Mimi binafsi, ninalaani vikali mauaji ya shahidi ndugu mujahid Ahmad Ghalib al-Rahwi, Waziri Mkuu na idadi ya mawaziri wa serikali ya wananchi wa Yemen mikononi mwa utawala wa Kizayuni wa Israeli, na tunaliita hili ni jinai nyingine iliyofanywa na utawala wa Israeli unaoelekea kuporomoka, kutokana na kuuwawa shahidi Waziri Mkuu na kundi kubwa la mawaziri wa serikali ya Yemen tunawapa pole ndugu zetu wa Ansarullah, hususan kiongozi wa Harakati ya Ansarullah Yemen Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi na watu wote mashujaa na wapambanaji wa Yemen, bila shaka, mapambano ya watu wa Yemen yamelifanya taifa la Israeli lenye ubaguzi wa rangi na mauaji ya kinyama kuwa dhaifu na kukata tamaa.
Chama cha Ustawi wa Kitaifa cha Afghanistan kinailaani vikali hatua hii ya fedheha ya Israeli, na kinayataka mataifa ya Kiislamu kufanya uamuzi thabiti dhidi ya uvamizi wa utawala haramu wa Israeli, la sivyo, kila siku tutashuhudia jinai zisizo na kikomo za Israeli katika Ukanda wa Ghaza, kusini mwa Lebanon na maeneo mengine ya Kiislamu, zikiwa na uungwaji mkono wa moja kwa moja na msaada wa Marekani.
Utawala wa muda wa Israeli hauna lengo jingine ila kufikia ndoto yake ya “kutoka Nile hadi Furati.” Waislamu na wapenda haki duniani wanapaswa kuchukua hatua za kivitendo dhidi ya mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israeli huko Yemen, Lebanon, Palestina iliyokaliwa kwa mabavu na Syria.
Chama cha Ustawi wa Kitaifa cha Afghanistan kinaiomba Umoja wa Mataifa kulaani kwa mara nyingine hatua ya uvamizi iliyofanywa na utawala wa jinai wa Israeli dhidi ya Yemen na Ukanda wa Ghaza na kuzuia mauaji haya ya halaiki ya kimbari.
Iwapo mataifa ya Kiislamu hayatatekeleza hatua za kivitendo, za kuzuia na kwa uratibu, basi kila siku Israeli itatekeleza uvamizi na mashambulizi ya mabomu dhidi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu moja baada ya nyingine.
Wassalaam
Muhammad Hasan Jafari
Katibu Mkuu wa Chama cha Ustawi wa Kitaifa cha Afghanistan
Maoni yako